Kuhusu Malazi

Kwa Nini Utumie Malazi?

Malazi ni jukwaa lako kuu la kutafuta na kutangaza hoteli, lodges, moteli, na nyumba za wageni kote nchini Tanzania. Imetengenezwa na Afrosoft Limited kupitia WantsMate, kwa ajili ya kurahisisha utafutaji wa huduma za malazi na huwasaidia watoa huduma kufikia wateja wengi zaidi.

Kwa Watoa Huduma: Wasaidie wateja wako wakufikie kwa urahisi zaidi!

Jisajili kwenye Malazi na upate faida hizi:

  • Fanya Biashara Kisasa – Nufaika na teknolojia ya kidijitali kwa usimamizi rahisi.
  • Fikia Wateja Zaidi – Wateja wanakupata kwa urahisi wakati wa kutafuta malazi
  • Simamia Biashara kwa Ufanisi – Dhibiti mauzo, matumizi, na faida kwa urahisi
  • Pokea Oda Wakati Wowote– Wawekee wateja wako vyumba vyao  mapema

Kwa Wateja: Usihangaike kutafuta huduma za malazi – suluhisho liko mkononi mwako!

Tumia simu yako upate malazi kwa haraka, popote ulipo. Kupitia Malazi, unapata:

  • Kuokoa Muda na Pesa – Tafuta malazi popote ulipo bila kuhangaika.
  • Chaguzi Nyingi Zaidi – Linganisha huduma, bei, na vifaa vinavyopatikana
  • Huduma za Karibu– Tumia anwani za makazi kupata huduma za malazi
  • Vitu Vilivyopotea – Wasiliana na mtoa huduma wako kuhusu vitu ulivyosahau

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), idadi ya watumiaji wa intaneti nchini Tanzania imeongezeka kwa asilimia 86.2, kutoka milioni 25.8 mnamo Januari 2020 hadi kufikia milioni 48 ifikapo Desemba 2024. Kati ya hao, watumiaji wa simu janja walikuwa takriban milioni 23.