Faragha ya Malazi

Katika jukwaa la Malazi, tunathamini faragha yako na tumejizatiti kulinda taarifa zako binafsi. Sera hii inaeleza jinsi tunavyokusanya, kutumia, na kulinda taarifa zako unapotumia jukwaa la Malazi, iwe kupitia tovuti yetu au Applikesheni ya simu ya WantsMate.
1. Taarifa Tunazokusanya
Tunaweza kukusanya taarifa zifuatazo unapoutumia jukwaa la Malazi:

  • Taarifa Binafsi – Jina, barua pepe, na namba ya simu.
  • Taarifa za Oda – Mapendeleo ya malazi, tarehe za kuingia na kutoka katika huduma ya malazi.
  • Taarifa za Kifaa na Matumizi – Anwani ya IP, aina ya kivinjari (browser), na jinsi unavyotumia jukwaa la malazi.

2. Jinsi Tunavyotumia Taarifa Zako
Tunakusanya na kutumia taarifa zako kwa madhumuni yafuatayo:

  • Kutangaza na kusaidia utafutaji wa huduma za malazi.
  • Kuwezesha malipo salama kwa watoa huduma.
  • Kuboresha uzoefu wa mtumiaji na huduma kwa wateja.
  • Kuimarisha usalama na kuzuia ulaghai kwa njia ya mtandao.

3. Kushiriki Taarifa & Usalama

  • Hatuziuzi taarifa zako binafsi kwa wahusika wengine.
  • Maelezo yako ya malipo yamefichwa (encrypted) na yanachakatwa kupitia njia salama.
  • Tunaweza kushiriki baadhi ya taarifa zako binafsi na watoa huduma za malazi pale unapohitaji kuweka oda ya chumba.

4. Haki Zako & Chaguo

  • Unaweza kurekebisha au kufuta taarifa zako binafsi katika jukwaaa la malazi wakati wowote.
  • Unaweza kujiondoa kwenye mawasiliano ya matangazo kutoka Afrosoft Limited.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na timu yetu ya usaidizi kupitia [email protected]