Masharti ya Malazi
Karibu kwenye jukwaa la MALAZI. Kwa kutumia tovuti yetu au aplikesheni ya simu ya WantsMate kwa ajili ya kutangaza au kutafuta huduma za malazi nchini Tanzania, unakubaliana na masharti yafuatayo:
1. Matumizi ya Jukwaa
- Malazi ni jukwaa la mtandaoni linalomikiwa na Afrosoft Limited linalowaunganisha wageni, wasafiri, wateja wengine na watoa huduma za malazi nchini Tanzania. Afrosoft Limited kupitia jukwaa la Malazi haimiliki wala kutoa huduma za malazi bali ni kiunganishi tu kati ya watoa huduma za malazi na wateja wao.
- Watumiaji (watoa huduma na wateja) wanapaswa kutoa taarifa sahihi kuhusu huduma na taarifa zao binafsi wanapotumia jukwaa la Malazi.
- Malazi ina haki ya kurekebisha mpangilio wa jukwaa, kuamua huduma zitakazotangazwa au kuondolewa, na kufuta maudhui yasiyohusiana na jukwaa.
2. Kuweka Oda & Malipo
- Oda za wateja zinaweza zinafanyiwa kazi upande wa mtoa Huduma ya Malazi
- Malipo (kwa watotoa huduma tu) yanachakatwa kwa kuzingatia usalama wa miamala kupitia malipo kwa njia ya simu mitandao yote nchini.
- Mteja anatakiwa kuwasiliana na Mtoa huduma ikiwa atahitaji kughairi Oda yake ya malazi.
3. Majukumu ya Mtumiaji
- Wateja wanapaswa kuheshimu sheria na kanuni za malazi
- Watoa huduma za malazi wanapaswa kutoa taarifa sahihi kuhusu malazi yao.
- Vitendo vya udanganyifu vitasababisha kufungiwa akaunti na kuondolewa katika jukwaa
4. Dhima & Migogoro
- Malazi ni jukwaa la kuunganisha watoa huduma na wateja na halihusiki na ubora wa huduma zinazotolewa na waendeshaji wa huduma za malazi wala matendo ya wateja.
- Migogoro kati ya wateja na watoa huduma za malazi inapaswa kutatuliwa moja kwa moja kati yao au kupitia timu yetu ya usaidizi wa jukwaa la Malazi.
5. Mabadiliko ya Masharti
- Malazi inaweza kurekebisha masharti haya mara kwa mara kwa ajili ya kuboresha huduma. Kuendelea kutumia jukwaa kunamaanisha unakubali mabadiliko yaliyopo.
Kwa maulizo au usaidizi, wasiliana nasi kupitia [email protected]